Rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini afariki dunia
11 Novemba 2021Fredrik Willem de Klerk, rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 85.De Klerk ambaye aliyemwachilia huru kutoka gerezani shujaa wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi Nelson Mandela, pamoja na Mandela aliyechaguliwa kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini walishinda kwa pamoja Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka wa 1993 kwa kuongoza kile kilichoonekana kuwa muujiza wa kuiongoa nchi kutoka utawala wa Kizungu.
Sikiliza zaidi hapa Taarifa ya wakfu wa De Klerk imesema alifariki dunia nyumbani kwake Fresnaye mjini Cape Town leo asubuhi baada ya kusumbuliwa na saratani. De Klerk alitangaza kuwa anaugua saratani wakati aliposherekea miaka 85 ya kuzaliwa mnamo Machi 18 mwaka huu. Amemuacha mke Elita, watoto Jan na Susan na wajukuu.