1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Namibia Hage Geingob afariki dunia

4 Februari 2024

Rais Hage Geingob wa Namibia amefariki leo Jumapili, 04.02.2024. Geingob ameaga dunia katika hospitali ya Lay Pohamba jijini Windhoek alikokuwa anapatiwa matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 82.

Windhoek, Namibia | Hayati Hage Geingob enzi za uhai wake
Aliekuwa Rais wa namibia Hage Geingob enzi za uhai wakePicha: Siphiwe Sibeko/REUTERS

Makamu wa Rais wa Namibia Nangolo Mbumba alitangaza kifo cha rais Hage Geingob na kusema kuwa kiongozi huyo aliaga dunia majira ya saa sita usiku.

Ofisi ya Rais wa Namibia imesema Kiongozi huyo wa Nambia aliaga dunia huku mkewe, Monica Geingos, na watoto wao wakiwa pembeni yake.

Soma pia:Rais wa Namibia Hage Geingob afariki dunia

Makamu wa Rais ambaye sasa anakaimu urais wa Namibia, ametoa wito wa utulivu, akisema baraza la mawaziri litakutana mara moja ili kutekeleza mipango muhimu ya serikali.

Marais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na William Ruto wa Kenya wametuma salamu za Rambirambi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW