Rais wa Nigeria atoa wito wa kusitishwa maandamano
4 Agosti 2024Matangazo
Katika hotuba kupita televisheni, Tinubu amewataka waandamanaji kusimamisha maandamano mengine yoyote na kutoa nafasi ya mazungumzo, ikiwa ni kauli yake ya mwanzo kwa umma tangu maandamano yalipoanza Alhamisi.
Katika hotuba hiyo alionesha kuwa amesikia kilio cha wananchi, kuelewa machungu waliyonayo na mfadhaiko uliosababisha waandamane na hivyo kutoa ahadi ya serikali kushughulikia kero zao.
Juma lililopita maelfu ya waandamanaji walianza kuingia barabarani kupinga sera za serikali na gharama kubwa ya maisha. Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeshutumu vikosi vya usalama kwa kuwaua takriban waandamanaji 13, huku polisi wakisema watu saba tu ndio waliofariki na kukana kuhusika na mauaji hayo.