Rais wa Palestina ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
26 Septemba 2010Matangazo
Katika hotuba yake kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani Rais wa Mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas amelaani kile alichokiita ''fikra za upanuzi na utawala'' za Israel.
Rais Abbas amesema Israel lazima ichague kati ya amani au ujenzi wa makaazi katika Ukingo wa Magharibi, kama inataka mafanikio katika mazungumzo ya amani ya kimataifa.
Muda wa kusimamisha ujenzi wa makaazi kwa kipindi cha miezi kumi katika Ukingo wa Magharibi unamalizika hii leo.
Rais Barack Obama wa Marekani na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wamesema Israel lazima iongeze muda huo na iendelee na mazungumzo ya amani yaliyoanza upya mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kukwama kwa karibu miaka miwili.