1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Peru achunguzwa kwa operesheni ya 'urembo' wa pua

6 Desemba 2024

Mwendesha mashitaka mkuu wa Peru amesema ofisi yake inaanzisha uchunguzi wa awali dhidi ya Rais Dina Boluarte kwa tuhuma za kukwepa majukumu yake.

Peru, Dina Boluarte
Rais Dina Boluarte wa Peru.Picha: Fernando Vergara/AP/picture alliance

Uchunguzi huo unatokana na kuibuliwa kwa kashfa ya kiongozi huyo kutoonekana hadharani kwa muda mnamo mwezi Juni na Julai mwaka jana, akiwa kwenye matibabu ya operesheni ya pua.

Siku ya Jumanne, waziri mkuu wa zamani, Alberto Otarola, aliiambia kamati ya bunge kwamba aliambiwa na Rais Boluarte kwamba alikuwa anakwenda kufanyiwa operesheni ya pua kutokana na tabu ya kupumua.

Soma zaidi: Kashfa ya saa za kifahari yawaangusha mawaziri 6 Peru

Kabla ya hapo, mitandao ya kijamii nchini Peru ilijaa uvumi kwamba rais huyo alitumia muda wa kazi kufanya operesheni ya urembo wa pua yake.

Mbali na kashfa hiyo, Boluarte anakabiliwa na shutuma za kutumia wadhifa kwa mambo ya anasa na kupokea rushwa ya saa za Rolex.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW