1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Peru kufanya ziara nchini China mwezi Juni

16 Mei 2024

Rais wa Peru Dina Boluarte anatarajiwa kufanya ziara nchini China mwezi ujao ili kukutana na mwenzake Xi Jinping.

Rais wa Peru Dina Boluarte
Rais wa Peru Dina BoluartePicha: Carlos Barria/REUTERS

Lima,

Rais wa Peru Dina Boluarte anatarajiNyumba ya rais wa Peru yavamiwa katika uchunguzi wa saa za kifahariwa kufanya ziara nchini China mwezi ujao ili kukutana na mwenzake Xi Jinping.

Nyumba ya rais wa Peru yavamiwa katika uchunguzi wa saa za kifahari

Hayo yameelezwa na Waziri wa kilimo wa Peru Angel Manero ambaye amesema suala la mauzo ya nyama ya ng'ombe kuelekea Beijing ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa na viongozi hao.

Manero amekadiria kuwa usafirishaji wa nyama ya ng'ombe kwenda China unaweza kukuza uchumi wa Peru kwa kiwango cha dola bilioni 3 hadi 4.

Ziara ya Boluarte itafanyika miezi michache kabla ya Peru kuwa mwenyeji mwezi Novemba wa mkutano wa kilele wa viongozi wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa nchi za Asia na Pacific- APEC, ambao Xi anatarajiwa kuhudhuria pamoja na viongozi wengine wa kanda hiyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW