SiasaPoland
Rais wa Poland kumtangaza waziri mkuu mpya
6 Novemba 2023Matangazo
Rais Andrzej Duda mshirika wa chama cha PiS alisema kabla ya uchaguzi kwamba atajaribu kuunda serikali ya chama kimoja kikubwa.
Kufuatia mashauriano na kutafakari kwa kina rais Duda amefanya maamuzi yake kuhusiana na kile kinachoonekana kuwa hatua ya mwanzo ya uteuzi wa serikali yake.
Soma pia:Muungano wa upinzani wafanikiwa wingi wa viti Poland
Kupitia ujumbe ulioandikwa katika mtandao wa X na mkuu wa shughuli za ofisi ya rais huyo,imebainika kwamba rais Duda anatarajiwa kulihutubia taifa jioni hii moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha taifa kutangaza waziri mkuu aliyemteua.
Miongoni mwa wanaotajwa kuwa nafasi kutangazwa kuchukuwa wadhifa huo ,ni waziri mkuu anayeondoka Mateusz Morawiecki, na Donald Tusk.