Rais wa Romania, Iohannis kuwania uongozi wa juu wa NATO
13 Machi 2024Matangazo
Katika hotuba yake kupitia televisheni amesema ameamua kuingia katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo, akiweka wazi uvumi uliodumu kwa muda mrefu kuhusu nia yake hiyo.
Aidha Rais Iohannis amesema Romania imekuwa nguzo ya utulivu kikanda na kuongeza kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kuiunga mkono NATO dhidi ya uvamizi wa Urusi. Mwanasiasa wa Romania Mircea Geoana kwa sasa anahudumu kama naibu katibu mkuu wa NATO.
Hatua hiyo inatarajiwa kutekeleza baada ya kumalizika kwa muhula wake wa pili madarakani katika msimu ujao wa mapukutiko.
Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte,ambaye pia anajiondoa katika siasa za kitaifa, anaonekana kuwa mstari wa mbele huku akiungwa mkono na Marekani.