Rais wa Russia alaumu Georgia na Ukraine kujiunga na NATO
25 Machi 2008Matangazo
Moscow.
Rais mteule wa Russia ameeleza kutoridhishwa kwake na uwezekano wa Ukraine na Georgia kujiunga na umoja wa kujihami wa NATO.
Dmitry Medvedev ameliambia gazeti la Financial Times katika mahojiano kuwa iwapo majimbo hayo mawili ya zamani ya iliyokuwa Urusi yatakuwa wanachama wa NATO , inaweza kuathiri usalama wa Ulaya.
Ukraine na Georgia zinauomba umoja huo wa NATO kuziruhusu kuwa wanachama wa mpango wa ushiriki, hatua inayoonekana kuwa hatua ya kwanza ya kujiunga na NATO. Suala la kuziingiza nchi hizo mbili linatarajiwa kujadiliwa katika mkutano mkuu wa NATO mjini Bucharest wiki ijayo ambapo rais anayeondoka madarakani Vladimir Putin amealikwa.