1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Rwanda aitaka nchi yake kujitegemea

6 Februari 2026

Rais wa Rwanda Paul Kagame ameirai nchi yake kujiandaa kujitegemea huku miito ikiongezeka nchini Marekani ya kuiwekea vikwazo zaidi kwa kushiriki kwake katika mzozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Rwanda Kigali 2025 | Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 mjini KigaliPicha: Cyrile Ndegeya/Anadolu/picture alliance

Akizungumza jana katika hafla moja iliyofanyika katika mji mkuu wa Rwanda Kigali, Kagame alionekana kujibu maswali kwa kusisitiza uhuru wa nchi hiyo.

" Kiwango cha vitisho tunavyokabiliana navyo kila siku. "Yaani, Tutafanya hivi usipofanya hivi, tutafanya vile usipofanya vile," unajua. Wakati mwingine unahisi kusongwa na vitisho vya aina hii ya lakini badala ya kusongwa na hayo yote, nitasongwa na kukaidi na kukuambia potelea mbali.”

Rwanda inasisitiza kuwa inahusika tu mashariki mwa Kongo ili kujilinda dhidi ya kundi la wanamgambo lililoundwa kutoka kwa wahusika waliobaki wa mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994, na kukanusha kuhusika moja kwa moja kijeshi licha ya ushahidi mkubwa kutoka kwa waangalizi wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW