Rais wa Senegal akutana na baraza la mawaziri
15 Februari 2024Rais wa Senegal Macky Sall amekutana na baraza lake la mawaziri jana, wakati akizidi kukabiliwa na shinikizo la ndani na kimataifa la kurejea katika kalenda ya uchaguzi uliocheleweshwa na kutatua mzozo mkubwa wa kisiasa.Umoja wa Ulaya waitaka Senegal kutoa hakikisho la uhuru wa kimsingi
Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa rais na baraza lake la mawaziri, ilizungumzia kidogo juu ya mzozo wa kisiasa unaoendelea. Ofisi ya rais, imechapisha video kwenye mitandao ya kijamii ikihimiza mazungumzo ya wazi ya kitaifa kabla ya uchaguzi.
Marekani, Ufaransa na Umoja wa Mataifa zimeunga mkono matakwa ya Wasenegali ya kutaka upigaji kura ufanyike haraka iwezekanavyo.
Kumekuwa na hofu kwamba mvutano huo unaweza kuenea na kusababisha ghasia zaidi. Watu watatu wameuawa katika maandamano, tangu Rais Sall alipotangaza kuchelewesha uchaguzi hadi Desemba.