1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Kandanda

Rais wa shirikisho la soka Italia atangaza kujiuzulu

2 Aprili 2026

Mkuu wa shirikisho la soka la Italia FIGC Gabriele Gravina ametangaza kujuzulu baada ya timu ya kandanda ya wanaume kushindwa kufuzu Kombe la dunia kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Italia- Mkuu wa shirikisho la soka la Italia FIGC Gabriele Gravina
Mkuu wa shirikisho la soka la Italia FIGC Gabriele GravinaPicha: picture-alliance/ZUMAPRESS/Lapresse/M. Alpozzi

Mkuu wa shirikisho la soka la Italia FIGC Gabriele Gravina ametangaza kujuzulu baada ya timu ya kandanda ya wanaume kushindwa kufuzu Kombe la dunia kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Gravina, ametangaza kuwa ataachia ngazi kufuatia mkutano uliofanyika makao makuu ya shirikisho hilo mjini Roma siku ya Alhamis.

Italia iliangukia pua katika mechi za kufuzu fainali ya Kombe la Dunia siku ya Jumanne, baada ya mikwaju ya penalti dhidi ya Bosnia na Hercegovina na hivyo kuikosa fainali ya michuano hiyo itakayofanyika msimu wa majira ya joto huko Marekani, Canada na Mexico.

Uchaguzi wa rais mpya wa shirikisho utafanyika Juni 22 huku jina la mkuu wa zamani wa kamati ya Olimpiki Giovanni Malago likitajwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW