1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Syria akutana na von der Leyen mjini Damascus

Josephat Charo
9 Januari 2026

Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa leo amekutana na rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.

Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa amekutana na rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen (pichani) mjini Damscus.
Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa amekutana na rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen (pichani) mjini Damscus.Picha: Nicolas Tucat/AFP/Getty Images

Chombo cha habari cha serikali ya Syria kimeripoti mkutano kati ya rais wa Syria Ahmed al-Sharaa na rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, huku von der Leyen akiwa afisa wa ngazi ya juu kabisa wa Umoja wa Ulaya kuwahi kuitembelea Syria tangu alipoondolewa madarakani kiongozi wa muda mrefu wa Syria Bashar al Assad.

Von der Leyen anafanya ziara ya kikanda pamoja na Antonio Costa, ambaye anaongoza Baraza la Ulaya.

Ziara yao inafuatia siku za mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Kikurdi katika mji wa Aleppo kaskazini mwa Syria yaliyowalazimisha maelfu ya raia kukimbia.

Wizara ya ulinzi ya Syria imetangaza leo inasitisha mapigano mjini Aleppo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW