Rais wa Syria Bashar al Assad afanya ziara rasmi Abu Dhabi
19 Machi 2023Matangazo
Rais wa Syria Bashar al Assad kwenye tiara hiyo ameandamana na mkewe Asma, na walipokelewa na Rais wa UAE Sheikh Mohammed bin Zayed al-Nahyan.
Ziara hiyo inafanyika wakati mataifa kadhaa ya kiarabu yametangaza nia yao ya kulegeza vikwazo dhidi ya Syria ambayo ilkuwa imetengwa na mataifa hiyo. Awali, Saudi Arabia, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE waliwaunga mkono waasi wanaopambana kuipindua serikali ya Assad.
Katika miaka ya hivi karibuni, Umoja wa Falme za Kiarabu umekua ukiimarisha uhusiano na Syria licha ya pingamizi la Marekani. Hatua hiyo inalenga kukabiliana na ushawishi wa Iran ambayo pamoja na Urusi, zinamuunga mkono Rais Bashar al Assad katika mzozo nchini mwake Syria.