Rais wa Syria Bashar Assad afanya ziara nchini China
22 Septemba 2023Matangazo
Rais wa Syria Bashar al Assad anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake rais wa China Xi Jinping katika siku ya pili ya ziara yake ya nchini humo.
Assad anafanya ziara hiyo, kwa mara ya kwanza tangu kufumuka kwa mgogoro nchini mwake mnamo mwaka 2011.
Ofisi ya rais wa Syria imesema kiongozi huyo amealikwa kufanya ziara hiyo na rais Xi Jinping.
Assad ameenda nchini China na maafisa waandamizi katika ujumbe wake. Kiongozi huyo wa Syria anatarajia kufikia mapatano na China juu ya msaada kwa nchi yake.
Hapo kesho Jumamosi rais huyo wa Syria atahudhuria sherehe ya ufunguzi wa michezo ya bara la Asia katika mji wa mashariki mwa China wa Hangzhou.