Rais wa Taiwan aapa kupinga kuzingirwa kwa kisiwa hicho
10 Oktoba 2024Matangazo
Lai amesema Beijing na Taipei haziko chini ya mamlaka au udhibiti wa mwingine na kwamba China haina haki ya kuiwakilisha Taiwan.
Kauli hii inajiri wakati China ikizidisha shinikizo la kijeshi na kisiasa katika kisiwa hicho kinachojitawala ambacho inadai ni sehemu ya ardhi yake na uhusiano wao umesalia kuwa tete chini ya uongozi wa Lai, ambaye aliingia madarakani mnamo Mei.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning, amekosoa kauli ya Lai kwamba "yuko tayari kwa lolote" ina nia mbaya ya kuongeza mvutano katika Mlango-Bahari wa Taiwan kwa ajili ya maslahi binafsi ya kisiasa.