1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuimarika kwa China ni changamoto kubwa kwa Taiwan

16 Juni 2024

Rais wa Taiwan Lai Ching-te amewaonya makadeti katika jeshi la nchi hiyo kwamba changamoto yao kuu ni kuimarika kwa nguvu ya China ambayo huenda ikakiondoa kisiwa hicho kinachojitawala chenyewe.

Taiwan | Lai Ching-te
Rais wa Taiwan Lai Ching-tePicha: Ann Wang/REUTERS

Akizungumza katika halfa ya kuhitimu kwa wanafunzi wa kijeshi, Lai alisema walimu wa wanafunzi hao wanapaswa kutambua changamoto na misheni ya enzi mpya, akisema China imekuwa ikiendelea kuyumbisha uhuru wa kisiwa hicho. 

China yaonya juu ya vita vya Taiwan baada ya luteka za kijeshi

China imekuwa ikidai kuwa kisiwa hicho ni sehemu ya eneo lake na viongozi wake wameendelea kusisitiza kauli zao katika miaka ya hivi karibuni kwamba kukichukua kisiwa hicho ni kitu kisichoepukika. 

China pia imekuwa ikiongeza shinikizo la kijeshi kwa kukizingira kisiwa hicho kwa ndege na meli za kivita siku kadhaa baada ya Lai kuapishwa rasmi kama rais wa Taiwan mwezi uliopita. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW