1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tanzania azungumzia kuporomoka kwa ghorofa

18 Novemba 2024

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezungumza Jumapili na vyombo vya habari akiwa nchini Brazil.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Rais wa Tanzania Samia Suluhu HassanPicha: Daniel Pier/NurPhoto/picture alliance

Rais Samia amesema hadi sasa hawajafahamu sababu za kuanguka kwa jengo hilo, huku akiyashukuru mashirika, wadau na wataalamu wa afya kwa msaada wao.

Aidha rais Samia amesema serikali itagharamia matibabu na kusaidia katika taratibu za mazishi. Kuporomoka kwa majengo hutokea katika baadhi ya  miji ya Afrika kutokana na udhaifu wa viwango vya ujenzi na wakati mwingine uzembe wa utekelezaji wa sheria.

Watu 13 wamethibitishwa kufariki na wengine zaidi ya 80 wamejeruhiwa nchini Tanzania, baada ya jengo la ghorofa kuporomoka Jumamosi iliyopita katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW