1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Tunisia Saied aapishwa kwa muhula wa pili

23 Oktoba 2024

Rais wa Tunisia Kais Saied ameapishwa kwa muhula wa pili, kufuatia mwezi mzima wa ukandamizaji na msururu wa kamatamata ya wapinzani wa kisiasa.

Rais aliyechaguliwa tena wa  wa Tunisia  Kais Saied picha huu ni kabla ya matokeo mapya
Rais aliyechaguliwa tena wa wa Tunisia Kais Saied picha huu ni kabla ya matokeo mapyaPicha: Fauque Nicolas/Images de Tunisie/ABACA/picture alliance

Wiki kadhaa baada ya kushinda tena uchaguzi kwa asilimia 97 ya kura, profesa huyo wa zamani wa sheria mwenye umri wa miaka 66 katika hotuba yake ya kuapishwa ametoa wito wa kile alichokiita mapinduzi ya kitamaduni ili kupambana na ukosefu wa ajira, vita dhidi ya ugaidi na kuangamiza ufisadi. Saied amesema katika hotuba yake kwa wabunge wa Tunisia kuwa lengo ni kuijenga nchi ambayo kila mmoja anaweza kuishi kwa heshima. Ushindiwa Saied katika uchaguzi wa Oktoba 7 ulijiri baada ya muhula wa kwanza wenye misukosuko amnapo alilivunja bunge la nchi hiyo, akaiandika upya katiba iliyoidhinishwa baada ya wimbi la mapinduzi ya umma lililopiga ulimwengu wa Kiarabu na akawafunga jela wakosoaji wake wa kisiasa, vyombo vya habari, biashara na asasi za kiraia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW