SiasaLebanon
Rais wa Ujerumani aahidi kuendelea kuisaidia Lebanon
16 Februari 2026
Matangazo
Steinmeier amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari sambamba na Rais wa Lebanon, Joseph Aoun kwamba Ujerumani itaendelea kushirikiana bega kwa bega na Lebanon.
Aidha ametoa wito kwa Lebanon na Israel kutimiza wajibu wao chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya mwaka 2025 ambayo aliyaelezea kama fursa kwa mataifa hayo yote mawili.
Makubaliano hayo kati ya Israel na Hezbollah yalifikiwa baada ya mapigano makali yaliyosababisha vifo vya watu 4,000 nchini Lebanon na 130 waliuawa Israel.