1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier aahidi kuisaidia Cape Verde

5 Oktoba 2023

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameahidi msaada kwa visiwa vya Cape Verde, ambavyo vimeathiriwa mno na mabadiliko ya tabianchi.

Frank-Walter Steinmeier
Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Rais huyo wa Ujerumani ametoa wito kwa Ujerumani kuwekeza zaidi katika visiwa hivyo vilivyopo takriban kilomita 500 magharibi mwa Afrika katika Bahari ya Atlantiki.

Steinmeier, ambaye kwa sasa yuko kwenye ziara ya kiserikali ya siku mbili nchini Cape Verde, alikaribishwa hapo jana kwa heshima za kijeshi na Rais José Maria Pereira Neves. Cape Verde imekuwa ikikumbwa mara kwa mara na majanga ya asili kama mafuriko na ukame.

Steinmeier  amehutubia hapo jana Bunge la nchi hiyo katika mji mkuu Praia na kusema, katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa, watu wa Cape Verde wanaweza kutegemea ujuzi wa matumizi ya teknolojia ya kisasa kutoka Ujerumani katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW