1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani ahimiza mageuzi ya sera ya wakimbizi

22 Septemba 2023

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametoa mwito wa kufanyika mageuzi katika sera ya Ulaya ya kuwahifadhi wakimbizi.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier(kulia) na rais wa Italia Sergio Mattarella (katikati) wakipiga selfie na kijana kutoka GambiaPicha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Steinmeier aliyasema hayo alipokuwa nchini Italia wakati ambapo kuna mvutano kati ya nchi hizo mbili kuhusu uhamiaji.

Rais wa Ujerumani amesema dunia imesonga mbele kutoka kwenye Mkataba wa Dublin na kwamba sheria hizo zimepitwa na wakati.

Amesema ana matumaini kuwa Ujerumani na Italia zitakutana tena na kuzungumza kwa pamoja kuhusu sera ya uhamiaji katika miezi ijayo.

Steinmeier: Ujerumani imefikia ukomo wa kupokea wahamiaji

Hivi majuzi, maelfu ya wahamiaji waliwasili katika kisiwa cha Lampedusa nchini Italia, na kusababisha mamlaka ya eneo hilo kutangaza hali ya hatari.

Wengi wa wanaowasili Italia huanzia Afrika Kaskazini kama sehemu yao ya kuondokea, huku Libya na Tunisia zikizingatiwa kama njia kuu ya wahamiaji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW