1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani aitembelea Uingereza

3 Desemba 2025

Ziara ya rais Frank Walter Steinmeier ni ya kwanza kuwahi kufanywa na kiongozi mkuu wa nchi wa Ujerumani nchini Uingereza kwa kipindi cha miaka 27

Rais  Frank-Walter Steinmeier akikaribishwa na mfalme Charles III.
Rais Frank-Walter Steinmeier akikaribishwa na mfalme Charles III.Picha: Carl Court/Getty Images

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amewasili leo mchana nchini Uingereza kwa ziara rasmi ya kiserikali, akiandamana pamoja na mkewe Elke Büdenbender.

Mfalme Charles wa tatu atawakaribisha rais Steinmeier na mkewe katika kasri la Windsor mwanzoni mwa ziara yao hiyo ya siku tatu, kwa kuwaandalia mapokezi ya kifahari na sherehe ambazo kwaasili, Ufalme huo wa Uingereza huwafanyia wageni wake mashuhuri.

Ujerumani yafanya Siku ya Maombolezo

Steinmeier, ni kiongozi wa kwanza wa Ujerumani kufanya ziara rasmi ya kiserikali nchini Uingereza katika kipindi cha miaka 27.

Baadae hivi leo atakutana na waziri mkuu Keir Starmer kwa mazungumzo yatakayojikita kwenye suala la vita vya Ukraine.

Siku ya Ijumaa, rais Steinmeier na mkewe watakwenda kwenye kanisa kuu la Coventry kukumbuka mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Manazi dhidi ya mji huo yaliyosababisha takriban, watu 568 kuuliwa,mwaka 1940.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW