1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ahimiza umoja

24 Desemba 2024

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ametumia hotuba yake ya kila mwaka ya Sikukuu ya Krismasi, kutoa wito kwa watu wa Ujerumani kusimama pamoja dhidi ya chuki

Deutschland Weihnachtsansprache des Bundespräsidenten Steinmeier
Picha: Annegret Hilse/AFP

Katika hotuba hiyo anayoitoa siku moja kabla ya sikukuu ya krismasi amezungumzia shambulio la hivi karubuni katika masoko ya krismasi katika mji wa Mashariki mwa Ujerumani wa Magdeburg. Ameziambia familia zilizoathirika kwamba haziko peke yao katika hili na kwamba taifa linasimama nao na kuomboleza nao wakati huu mgumu.

Steinmeier, pia aliwapongeza maafisa wa usalama na wataalamu wa afya kwa kazi yao kubwa baada ya shambulio hilo, akitoa wito zaidi kwa wajerumani kutogawanywa na matukio haya akisema chuki na vurugu havipaswi kupewa nafasi katika jamii. 

Ijumaa ya tarehe 20 Desemba mwanamume mmoja mwenye asili ya Saudi Arabia aliyetambuliwa kwa jina la Taleb A, alivurumisha gari katikati ya umati wa watu kwenye soko la Krismasi na kusababisha mauaji ya watu 5 na wengine zaidi ya 200 walijeruhiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW