1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier: Ujerumani itasimama na Israel dhidi ya Hamas

27 Novemba 2023

Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema Ujerumani itasimama na Israel katika vita vyake Ukanda wa Gaza

Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier aliyeko ziarani nchini Israel amesema nchi yake itatoa msaada kuzijenga upya jamii za Israel zilizopata uharibifu kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya kundi la Hamas ya oktoba 7.

Rais huyo wa Ujerumani ameyasema hayo hii leo wakati akilitembelea eneo la Kibbutz Bee'ri ambalo ni moja ya maeneo yaliyolengwa na wanamgambo hao wa Kipalestina.

Amesema Ujerumani itatowa dola zaidi ya milioni 7 mwaka ujao kusaidia ujenzi wa eneo hilo.

Soma pia:Muda wa usitishaji vita Gaza huenda ukarefushwa

Jana akiwa Jerusalem pamoja na rais wa Israel Isaac Herzog Steinmeier alisema Ujerumani itaendelea kuiunga mkono Israel katika vita vyake Ukanda wa Gaza, akisisitiza kwamba Ujerumani haiko tu na Israel kama muhanga wa ugaidi bali, mshikamano wa nchi hiyo pia uko kwaajili ya kuisadia Israel kujilinda na kupambana dhidi ya kitisho kinachoikabili.

Kiongozi huyo wa Ujerumani pia amesema ni muhimu kuwalinda raia katika ukanda huo wa Gaza na kuwapatia mahitaji ya msingi ya kibinadamu, kwa mujibu wa sheria ya kiutu ya kimataifa.