1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky awatembelea wanajeshi wake walio vitani

4 Februari 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatembelea wanajeshi walioko eneo la mapambano makali katika kijiji cha Robotyne kilicho kusini mwa Ukraine ambacho Kyiv ilichukua tena udhibiti wake kutoka kwa vikosi vya Urusi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Picha: Thomas Coex/AFP

Kupitia mtandao wa kijamiiZelenskyaliwasifu wapiganaji wake walioko kwenye mstari wa mbele wa mapambano katika eneo hilo na kuongeza kuwa ni muhimu kufanya kila linalowezekana ili kufanikisha ushindi wa mapema katika eneo hilo.

Eneo la Robotyne kusini mwa Zaporizhzhia limeshuhudia mashambulizi makali ya pande mbili na moja wapo ya maeneo ya kimkakati upande wa kusini mwa Ukraine.

Katika hatua nyingine jeshi la Ukraine limesema kuwa limezima mashambulio 27 ya Urusi karibu na mji wa Avdiivka ambayo mosco imejaribu kuweka chini ya udhibiti kwa miezi kadhaa.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema mapema wiki hii kwamba vikosi vya Moscow "vimefika kwenye viunga vya Avdiivka".

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW