1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vladimir Putin: Uasi wa mamluki wa Wagner ni usaliti

24 Juni 2023

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema katika hotuba ya dharura leo Jumamosi kuwa maasi ya kutumia silaha ya kikosi cha mamluki cha Wagner ni uhaini na yeyote aliyebeba silaha dhidi ya jeshi la Urusi ataadhibiwa.

Russland | TV Ansprache Putin
Picha: via REUTERS

Rais Putin ameahidi  kufanya kila linalopasa kuilinda Urusi na ameeleza kwamba hatua madhubuti zitachukuliwa ili kurejesha utulivu kwenye mji wa Rostov-on-Don ulio kusini mwa Urusi ambako kamanda wa kundi la mamluki wa Wagner, Yevgeny Prigozhin amesema wapiganaji wake wapatao elfu 25 wanadhibiti sehemu zote muhimu za kijeshi. Prigozhin ameapa kuuangusha uongozi wa kijeshi wa Urusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW