Vladmir Putin aahidi kuendelea kuisaidia Afrika
10 Novemba 2024Matangazo
Katika hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov, Putin amesema nchi yake itaendelea kutoa msaada katika sekta mbalimbali zikiwemo maendeleo endelevu na mapambano dhidi ya ugaidi na itikadi kali.
Soma zaidi:Urusi yaahidi kulisaidia kikamilifu bara la Afrika
Msaada huo utaelekezwa pia kukabiliana na uhaba wa chakula na matokeo ya majanga ya asili barani Afrika. Mkutano huo wa siku mbili ulioanza Jumamosi umewahusisha mawaziri na maafisa wa ngazi ya juu kutoka Afrika na unatajwa kuwa nafasi nyingine kwa Urusi kutangaza malengo yake ya kutaka kuona ulimwengu usioendeshwa na upande mmoja wa dunia. Taifa hilo hivi karibuni liliandaa pia mkutano wa kilele wa mataifa yanayokuwa kiuchumi ya BRICS.