1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUzbekistan

Rais wa Uzbekistan ashinda muhula mwingine madarakani

10 Julai 2023

Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev ameshinda muhula wa tatu madarakani baada ya uchaguzi uliofanyika jana, matokeo yanayomwezesha kuendelea kuitawala nchi hiyo ya Asia ya Kati hadi mwaka 2030.

Uzbekistan, Shavkat Mirziyoyev
Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev wakati akipiga kuraPicha: Press service of the President of Uzbekistan/REUTERS

Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev ameshinda muhula wa tatu madarakani baada ya uchaguzi uliofanyika jana, matokeo yanayomwezesha kuendelea kuitawala nchi hiyo ya Asia ya Kati yenye utajiri mkubwa wa mafuta hadi mwaka 2030.

Matokeo ya awali yanaonesha Mirziyoyev aliyekuwa akichuana na wagombea wengine watatu wasio na umaarufu mkubwa amepata ushindi wa asimilia 87 ya kura.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 65 aliahidi mageuzi makubwa wakati wa kampeni ikiwemo kukaribisha uwekezaji wa kigeni na kuifufua sekta ya utalii ya taifa hilo lililokuwa sehemu ya Dola ya Kisovieti.

Soma pia: Uzebkistan yaidhinisha mabadiliko yatakayorefusha utawala wa rais

Rais Xi Jinping wa China na Vlamidir Putin wa Urusi wamekuwa viongozi wa kwanza wa ulimwengu kutuma salamu za pongezi kwa Mirziyoyev ambaye anaiongoza Uzbekistan tangu mwaka 2016.

Ushindi wake unafuatia mabadiliko ya katiba yaliyofanyika mwaka huu yaliyomruhusu kuwania tena kiti cha urais kwa mihula mingine miwili ya miaka saba.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW