1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Rais wa zamani Ahmadnejad ajisajili kuwania urais Iran

Saleh Mwanamilongo
2 Juni 2024

Rais wa zamani wa Iran Mahmoud Ahmadinejad amejisaliji Jumapili kugombea nafasi ya urais baadaye mwezi huu.

Rais wa zamani wa Iran Mahmud Ahmadinejad kuwania tena urais
Rais wa zamani wa Iran Mahmud Ahmadinejad kuwania tena uraisPicha: dpa/AP/picture alliance

Ahmadinejad, mwenye umri wa miaka 67, alishikilia wadhifa huo kwa mihula miwili mfululizo kuanzia mwaka 2005 hadi 2013, kipindi ambacho kilikuwa na msuguano na nchi za Magharibi hasa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na matamshi yake ya kuichokoza Israel.

Spika wa zamani wa bunge Ali Larijani, Gavana wa zamani wa benki kuu nchini humo Abdolnaser Hemmati ni miongoni mwa watu 13 waliojisajili kugombea nafasi hiyo.

Baada ya usajili wagombea watachujwa na Baraza la viongozi wa kidini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW