1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa zamani atuhumiwa jaribio la mapinduzi Sierra Leone

13 Desemba 2023

Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, ni miongoni mwa watuhumiwa wa kile serikali ya nchi hiyo inachosema ni "jaribio la mapinduzi" la mwezi uliopita.

Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma (kushoto).
Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma (kushoto).Picha: AP

Mkuu wa polisi wa taifa hilo la Afrika Magharibi, Fayia Sellu, amesema kwa mujibu wa maelezo aliyoandikisha kwa hiyari yake, Koroma anatuhumiwa kushiriki jaribio hilo.

Jumamosi iliyopita, mamlaka nchini Sierra Leone zilisema rais huyo wa zamani alikuwa kwenye kizuizi cha nyumbani wakati akifanyiwa mahojiano.

Soma zaidi: Aliyepanga mapinduzi Sierra Leone akamatwa

Siku ya Jumanne (Disemba 12), serikali kupitia waziri wake wa habari, Chernor Bah, ilithibitisha kuwa sasa Koroma ni mtuhumiwa rasmi.

Kundi la watu wenye silaha lilivamia ghala la silaha la jeshi, kambi mbili, jela mbili na vituo viwili vya polisi mapema ya tarehe 26 Novemba, ambapo kwenye makabiliano na vyombo vya usalama, watu 21 waliuawa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW