1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa zamani wa Botswana aitwa mahakamani

20 Aprili 2022

Rais wa zamani wa Botswana, Ian Khama, ametakiwa kufika mbele ya mahakama mjini Gaborone kujibu makosa 13 ya jinai, likiwemo la kumiliki silaha kinyume na sheria

Ian Khama
Picha: picture-alliance/ dpa

Hati ya wito iliyotolewa na mahakama, ambayo shirika la habari la AFP imeiona, inaonesha Khama anakabiliwa pia na makosa ya kupokea mali ya wizi na kughushi nyaraka za umiliki wa silaha.

Kwa sheria ya Botswana, kumiliki bunduki kinyume na sheria kuna adhabu ya kifungo cha hadi miaka 10 gerezani.

Haijafahamika iwapo Khama, ambaye alikuwa rais wa Botwasa kwa miaka 10 hadi mnamo 2018, ataitikia wito huo wa kufika mahakamani. 

Katika shauri hilo, Khama, ambaye sasa anaishi nchini Afrika Kusini alikokimbilia Novemba mwaka uliopita, anashtakiwa pamoja na mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi pamoja na mkuu wa polisi aliyefutwa kazi.

Chanzo: afp