1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Rais wa zamani wa Brazil agunduliwa na saratani ya ngozi

18 Septemba 2025

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro amegunduliwa kuwa na saratani ya ngozi baada ya kulazwa hospitalini kufuatia maradhi tofauti.

Brasilia 2025 | Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro
Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro akiwa mjini BrasiliaPicha: Leandro Chemalle/TheNEWS2/ZUMA/picture alliance

Hayo yameelezwa na daktari wake Claudio Birolini aliyewaambia waandishi wa habari kwamba Bolsonaro alipelekwa hospitalini kutokana na matatizo ya kutapika, kizunguzungu na shinikizo la damu.

Matatizo hayo ya kiafya yanajiri baada ya mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 70 kuhukumiwa wiki iliyopita kifungo cha miaka 27 jela kwa kosa la kupanga njama ya mapinduzi.

Wanasheria wa Bolsonaro wanatarajiwa kutumia hali hii ya kiafya kama kigezo cha kufanya maombi ya mteja wao kupewa kifungo cha nyumbani badala ya kulazimika kukaa gerezani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW