1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Bolsonaro aanza kutumikia kifungo cha miaka 27

26 Novemba 2025

Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro jana Jumanne alianza kutumikia kifungo cha miaka 27 jela kwa kuongoza jaribio la mapinduzi.

Brazil São Paulo 2024 | Jair Bolsonaro akiwa katika mkutano wa Siku ya Uhuru
Rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro aanza kutumikia kifungo cha miaka 27 jela kutokana na tuhuma za jaribio la mapinduziPicha: Nelson Almeida/AFP

Jaji wa Mahakama Kuu Alexandre de Moraes, aliyeongoza kesi hiyo aliatoa uamuzi wa kumbakisha Bolsonaro kizuizini baada ya kukamatwa mapema Jumamosi.

Bolsonaro hatakaribiana na wafungwa wengine wachache wanaozuiwa katika makao makuu ya polisi ya shirikisho.

Jaji De Moraes alichukua uamuzi huo wakati upande wa utetezi ukiwa umemaliza rufaa zote. Hata hivyo, mawakili wa Bolsonaro wameahidi kuendelea kuwasilisha maombi ya kifungo cha nyumbani kutokana na afya mbaya ya kiongozi huyo wa zamani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW