SiasaGhana
Rais wa zamani wa Ghana John Mahama ashinda uchaguzi wa rais
9 Desemba 2024Matangazo
Tume ya uchaguzi ya Ghana haijatangaza matokeo rasmi lakini Mahamudu Bawumia, Makamu wa rais wa Ghana na mgombea wa chama tawala cha New Patriotic Party (NPP) amekubali kushindwa.
Kushindwa kwake kunahitimisha miaka minane ya uongozi wa chama cha NPP chini ya Rais Nana Akufo-Addo , ambaye muhula wake wa mwisho ulikumbwa na msukosuko mbaya zaidi wa kiuchumi, ambapo wapiga kura wameonekana kukiadhibu chama tawala kwa jinsi serikali ilivyoshughulikia matatizo ya kiuchumi hasa mfumuko wa bei.
Mahama aliyewahi kuwa rais wa Ghana kuanzia mwaka 2012 hadi mwanzoni mwa mwaka 2017, ameahidi kulifufua upya taifa hilo la Afrika Magharibi kwa kutoa msaada kwa wafanyabiashara vijana na wakulima.