Rais wa zamani wa Juan Orlando Hernandez Honduras
16 Februari 2022Matangazo
Kukamatwa kwake kumetokea chini ya wiki tatu baada ya Hernandez kuachia madaraka na madai ya miaka kadhaa ya waendesha mashitaka wa Marekani yanayomuhusisha na walanguzi wa dawa za kulevya.
Hapo jana, jaji wa mahakama ya juu ya haki nchini Honduras aliyeteuliwa kushughulikia kesi yake, alisaini kibali cha kukamatwa kwa rais huyo wa zamani Juan Orlando Hernandez.
Hernandez anatuhumiwa kula njama na makundi ya kusafirisha dawa za kulevya na ufisadi katika taasisi nyingi za umma, kuzorota kwa shughuli za kijamii na kudhoofisha matumizi ya haki nchini Honduras.
Chanzo: reuters