Nicolas Sarkozy arudi tena mahakamani
7 Aprili 2026
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amerudishwa tena mahakamani leo Jumanne, kusikiliza kesi inayomuandama kuhusiana na tuhuma kwamba kampeini yake ya uchaguzi mwaka 2007 ilifadhiliwa kwa njia haramu kwa fedha kutoka Libya.
Kiongozi huyo wa zamani wa Ufaransa alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na mpango wa kujipatia fedha kutoka serikali ya aliyekuwa rais wa Libya Muammar Gadhafi kwa ahadi ya kumuunga mkono kisiasa na kidioplomasia.
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kwenda jela Jumanne
Hata hivyo mahakama ya rufaa mjini Paris baadae iliagiza aachiwe huru kusubiri kesi hii mpya ya rufaa,ambayo imepangwa kuendelea hadi mwezi Juni.
Kesi hiyo inatarajiwa kupitia upya ushahidi wote uliowasilishwa, unaohusiana na Sarkozy pamoja na washtakiwa wenzake 9 wakiwemo watatu waliokuwa mawaziri.
Sarkozy amekanusha mashtaka yanayomuandama akidai yalichochewa kisiasa.