1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Medvedev asema jeshi la nchi hiyo litaingia Kiev na Lviv

24 Machi 2023

Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev amesema vikosi vya nchi hiyo huenda vikaingia mpaka mji mkuu wa Ukraine, Kiev, au mji wa Lviv.

Russland | Dmitri Medwedew
Picha: Alexei Maishev/TASS/IMAGO

Medvedev amenukuliwa na shirika la habari la RIA Novosti hii leo Ijumaa akisema kwamba hawawezi kuondowa uwezekano wa kuingia kwenye miji hiyo ya Ukraine kuondowa kile alichokiita maambukizo.

Kauli hiyo imekuja wakati hapo jana viongozi wa Umoja wa Ulaya, waliihakikishia tena Ukraine uungaji mkono na kufungua mlango wa kuiwekea vikwazo vipya Urusi.

Soma pia: Rais wa zamani wa Urusi aionya Jumuiya ya Kujihami ya NATO kuhusu vita vya nyuklia

Katika mkutano mjini Brussels jana, Umoja huo uliahidi kuongeza shinikizo dhidi ya Urusi. Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja huo, Ursula von der Leyen, alitangaza kampeni ya kimataifa kupitia juhudi za Poland ya kuwatafuta na kuwarudisha nchini Ukraine watoto waliosafirishwa kwa nguvu nchini Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW