1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Ruto ateua msimamizi wa wizara baada ya kuvunja baraza

18 Julai 2024

Rais wa Kenya William Ruto amemteua waziri wake wa mambo ya nje Musalia Mudavadi kuwa "kaimu msimamizi wa wizara zote” nchini humo wiki moja baada ya kulivunja baraza lake la mawaziri.

Kenya Nairobi | Rais William Ruto
Rais William Ruto akitangaza kukopa zaidi baada ya kuachana na mapendekezo tata ya bajeti ya mwaka 2024 yaliyosababisha maandamano makubwa na hatimaye kuvunjwa baraza la mawaziriPicha: TONY KARUMBA/AFP

Kulingana na notisi ya gazeti la serikali iliyotiwa saini na Rais Ruto na kutolewa jana Jumatano, Mudavadi sasa atazisimamia wizara zote 21.

Mudavadi, ambaye pia anashikilia nyadhifa za waziri kiongozi na waziri wa mambo ya nje, pamoja na makamu wa Rais Rigathi Gachagua ndio walionusurika shoka la kuondolewa kwenye baraza la mawaziri mnamo Julai 11.

Taifa hilo la Afrika Mashariki lilikumbwa na maandamano baada ya bunge la kitaifa kupitisha mswada tata wa fedha uliotoa mapendekezo ya kuongeza ushuru.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW