1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Xi aongeza juhudi za kuinadi China katika utandawazi

21 Novemba 2024

Rais wa China Xi Jinping, ameanzisha kampeni madhubuti ya kidiplomasia kuifanya nchi yake kuwa kinara wa utandawazi na ushirikiano wa kimataifa.

 Lula da Silva na  Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping na rais wa Brazil Lula da Silva Picha: Ricardo Stuckert/PR

Rais wa China Xi Jinping, ameanzisha kampeni madhubuti ya kidiplomasia kuifanya nchi yake kuwa kinara wa utandawazi na ushirikiano wa kimataifa, katika ulinganisho na ajenga ya Donald Trump ya kutanguliza maslahi ya Marekani, baada ya Mrepublican huyo kuchaguliwa tena kwa muhula wa miaka minne.

soma: Rais Xi Jinping aanza ziara rasmi nchini Brazil

Kupitia mikutano ya kimataifa kama ya APEC na G20, Xi ameiwasilisha China kama mshirika thabiti na wa kuaminika, akilenga kuimarisha mahusiano na nchi za Kusini mwa Dunia na kuwashawishi washirika wa Marekani barani Ulaya walio na wasiwasi.

Hata hivyo, mvutano usioisha kuhusu biashara, migogoro ya maeneo, na mashaka juu ya ushawishi unaoongezeka wa Beijing vinaendelea kutia kiwingu juhudi hizi. Wachambuzi wamebainisha kuwa hata China ilipojaribu kurekebisha msimamo wake wa kidiplomasia, udhaifu wa kiuchumi na mazingira mapana ya kijiografia bado vinatoa changamoto kubwa kwa matarajio yake.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW