Xi arejea wito wa suluhisho la madola mawili mzozo wa Gaza
30 Mei 2024Matangazo
Xi alikuwa akizungumza kwenye mkutano kati ya China na viongozi wa mataifa ya kiarabu unaofanyika leo mjini Beijing.
Soma pia:Vifaru vya kijeshi vya Israel vyaendeleza mashambulizi Rafah
Amesema tangu Oktoba mwaka jana mzozo kati ya Israel na Palestina umetanuka na kuwatumbukiza watu kwenye masaibu ya kutisha.
“Vita haviwezi kuendelea bila kikomo. Haki haiwezi kukosekana daima. Na iwapo kuna nia, shabaha ya kupatikana suluhu kwa kuundwa madola mawili haiwezi kudhoofishwa" Alisema Xi.
Kwenye mkutano huo wa mjini Beijing unaohudhuriwa na viongozi wa Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Tunisia, Rais Xi ameahidi kwamba nchi yake itatoa mchango wa angalau dola milioni 72 kusaidia utoaji misaada kwa ajili ya Ukanda wa Gaza.