1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Xi akutana na rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Beijing

13 Septemba 2023

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Venezuela Nicolas Maduro wamefanya mazungumzo mjini Beijing, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya China Xinhua.

China Staatsbesuch Nicolas Maduro
Picha: picture-alliance/Xinhua/Y. Dawei

Xinhua imeripoti pia kwamba rais Xi atamkaribisha kwenye sherehe mwenyeji wake katika ukumbi wa jengo la serikali la shughuli za bunge. Rais Maduro aliwasili jana Jumanne Beijing  baada ya kuitembelea miji kadhaa ya China ikiwemo Shanghai.

Urusi, China zamkingia kifua Maduro

Rais Maduro ambaye ziara yake nchini China itamalizika Alhamisi anataka nchi yake Venezuela ipate uanachama katika jumuiya ya nchi zinazoinukia kiuchumi ya BRICS.

China ni mkopeshaji mkubwa wa Venezuela na imekuwa na uhusiano wa karibu na nchi hiyo ambayo imetengwa kidiplomasia.