Rais Xi Jinping asifu uhusiano wa China na Indonesia
1 Aprili 2024Rais wa China Xi Jinping amemwambia Prabowo katika mazungumzo mjini Beijing kuwa mahusiano baina ya mataifa hayo ya Asia yameingia katika hatua mpya ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja, yenye ushawishi wa kikanda na kimataifa na kwa ajili ya amani na maendeleo ya dunia.
Aidha Xi amemsisitizia rais mteule Prabowo ambae anatarajiwa kuapishwa mnamo mwezi Oktoba kuwa ufunguo wa uhusiano thabiti baina yao "utazingatia kuaminiana, uhuru wa kuchagua, kusaidiana pamoja na usawa na haki".
Soma pia: Prabowo Subianto ashinda uchaguzi wa urais Indonesia
Prabowo anafanya ziara yake ya kwanza kwa mshirika mkuu wa kibiashara wa Jakarta tangu ushindi wake katika uchaguzi mwezi uliopita.
China imewekeza mabilioni ya dola katika miradi mikubwa ya kimkakati nchini Indonesia ikiwamo reli ya mwendo kasi.