1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Rais Xi wa China anaanza ziara Korea Kaskazini

8 Juni 2026

Rais Xi Jinping wa China anaelekea Korea Kaskazini leo Jumatatu kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kuimarisha zaidi mahusiano na taifa hilo jirani lenye silaha za nyuklia.

China Beijing 2026 | Rais Xi Jinping wa China
Rais Xi Jinping wa China.Picha: Maxim Shemetov/AP Photo/picture alliance

Hiyo itakuwa ziara ya kwanza ya Xi nchini Korea Kaskazini katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

Katika makala iliyoandikwa na kiongozi huyo wa China na kuchapishwa leo hii, Xi amesema ni sera isiyoyumba ya utawala mjini Beijing kuimarisha mahusiano na Korea Kaskazini. Pia amesema nchi hizo mbili zitafanya kazi pamoja kupambana na tabia za ubabe na kuongezeka mbio za kuunda silaha mambo aliyoyataja kuwa kitisho kwa usalama na udhabiti wa kanda hiyo.

Akiwa mjini Pyongyang, Xi atakutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ambaye alikutana naye mara ya mwisho Septemba mwaka jana alipomwalika Kim nchini China kwa gwaride kubwa la kijeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW