SiasaAsia
Rais Xi wa China awasili Cambodia kwa ziara ya siku mbili
17 Aprili 2025
Matangazo
Xi atakutana na viongozi mbalimbali wa Cambodia ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Hun Manet aliyesema hivi majuzi kuwa China ni mshirika muhimu ambaye ameisaidia nchi hiyo kiuchumi na kijamii.
Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza tangu mwaka 2016, itahitimisha safari ya Xi kwenye nchi tatu za kusini-mashariki mwa Asia iliyozijumuisha Vietnam na Malaysia.
Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa ikiongeza ushawishi wake katika eneo hilo kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa kiuchumi.