1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaAsia

China na Ujerumani zaonya dhidi ya vizuizi vya kibiashara

17 Aprili 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alikutana na Rais wa China Xi Jinping katika siku ya mwisho ya ziara yake ya siku tatu mjini Beijing. China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Ujerumani.

Kansela Scholz ziarani China
Kansela Scholz anasema ushindani kati ya China na Ujerumani unapaswa kuwa wa hakiPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Viongozi hao wawili walisisitiza haja ya kuepukana na sera za ulinzi wa masoko. Xi alisema uhusiano na Ujerumani utaendelea kukua kama mataifa yote yataheshimiana na kutafuta maelewano.

Soma pia: Mkakati wa Ujerumani wa China wakaribishwa Taiwan, wakosolewa Beijing

Scholz alisema anataka kufanya kazi na uongozi wa China ili kuyaboresha mazingira ya makampuni ya Ujerumani nchini China. Siku ya Jumatatu, Scholz alisema kuwa ushindani kati ya China na Ujerumani unapaswa kuwa wa haki na akaonya Beijing dhidi ya kutekeleza sera za ulinzi wa masoko katika sekta ya magari.

Hii ilikuwa ziara ya kwanza ya Kansela Scholz nchini China tangu Berlin ilipoutangaza mkakati wake wa kibiashara mwaka wa 2023. Mkakati huo unalenga kuhakikisha kuwa Ujerumani haiitegemei sana China, ambayo ndio nchi ya pili kubwa kiuchumi ulimwenguni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW