Rais Zelensky afanya ziara Berlin
14 Aprili 2026
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz ametangaza mipango ya kushirikiana na Ukraine katika teknolojia ya utengenezaji droni na mifumo ya ukusanyaji taarifa kwenye maeneo ya vita.
Merz ametangaza mpango huo leo kufuatia mkutano wake wa rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini Berlin ambako pia aliitolea mwito Kiev kuendelea na mageuzi yenye lengo la kuifikisha Ukraine katika hatua ya kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Ujerumani na Ukraine zatia saini mikataba ya ushirikiano
''Tunataka kuiongoza Ukraine kuhusu namna inavyoweza kujisogeza karibu na Umoja wa Ulaya,hatua kwa hatua. Huu hautokuwa uanachama wa daraja la pili bali utakuwa ni mchakato utakaoipleka karibu na kufikia hatua hiyo.
Rais Volodymyr Zelensky amesema amejadili pamoja na kiongozi huyo wa Ujerumani kuhusu mpango wa Ulaya wa kuwa na mfumo wa pamoja wa kuzuia makombora ya masafa marefu na utengenezaji wa Droni.
Kansela Friedrich Merz pia ameunga mkono hatua ya wakimbizi wa Ukraine walioko Ujerumani kurejea nyumbani.