1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Zelensky ataka Marekani iipigie chapuo kuingia NATO

1 Desemba 2024

Rais Volodymyr Zelenskiy ameitolea mwito Marekani kuushawishi Ulaya wenye mashaka, kwamba Ukraine inapaswa kukaribishwa kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO.

Der ukrainische Präsident Wolodymyr Selenskyj
Rais wa Ukrain Volodymyr Zelenskyy, wakati wa maelezo mafupi juu ya hali vita Novemba 18, 2024,Picha: IMAGO/ZUMA Press Wire

Zelensky amesema katika mkutano wake na waandishi habari mjini Kiev, kwamba hatua yoyote ya kuialika nchi yake kujiunga na NATO inapaswa kuhusisha maeneo yote ya nchi hiyo isipokwa yale yanayokaliwa yanayokabiliwa na vita vinavyoendelea. Kwa mujibu wa kiongozi huyo,Ukraine inahitaji kuwemo ndani ya NATO ili iendelee kuwepo,wakati ikipambambana na Urusi.  Ametowa mwito wa kupatiwa silaha,na hakikisho la kiusalama kabla ya kukaa kwenye meza ya mazungumzo na Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW