1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Rais Zelensky aitembelea Donetsk inayokumbwa na vita

6 Desemba 2022

Rais wa Ukraine ametembelea eneo la Donetsk linalokumbwa na vita Mashariki mwa Ukraine, akisema mapigano yamepamba moto, huku wanajeshi wa Urusi wakisonga mbele kutaka kuudhibiti mji wa kiviwanda wa Bakhmut.

Ukraine | Wolodymyr Selenskyj in Cherson
Picha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Ziara ya Volodymyr Zelensky imekuja wakati rais wa Urusi Vladimir Putin, akifanya mkutano na Baraza lake la Usalama wakati taifa lake likishambuliwa hivi karibuni kwa makombora dhidi ya kambi zake za kijeshi. Vita vya Ukraine vimechukua mkondo mpya kwa kuelekea katika mji wa Donbas  baada ya wanajeshi wa Ukraine kuutwaa tena mji wa Kusini wa Kherson kutoka mikononi mwa wanajeshi wa Urusi.

Zelensky alionekana katika vidio akiwa amevalia koti zito la baridi akisimama karibu na  bango kubwa lililokuwa na rangi za bendera za Uturuki lililoandikwa jina la Slovianks,  akitoa wito wa kunyamaa kwa dakika moja kutoa heshima kwa wanajeshi wake waliouwawa ktika vita vinavyoendelea.

"Vita vya Mashariki ya Ukraine kwa sasa ni vigumu na ninafarijika kusimama hapa na wanajeshi wetu wanaoilinda nchi yetu hapa Donbas. Naamini mara nyengine tutakutana mjini Donetsk na Lugansk na hata katika eneo lililonyakuliwa na Urusi la Krimea," alisema rais Zelensky.

Ukraine yapambana kurudisha umeme baada ya mashambulizi

Wanajeshi wa Urusi na washirika wake wanadhibiti maeneo ya Donetsk and Lugansk tangu mwaka 2014 wakati mapigano ya watu wanaotaka kujitenga yalipoanza.

Rais huyo wa Ukraine ametembelea maeneo mengi ya vita nchini Ukrtaine ikiwa ni miezi tisa baada ya Urusia kulivamia taifa hilo la muungano wa zamani wa kisovieti.

Putin akutana na Baraza lake la usalam kujadili usalama wa taifa lake

Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: SPUTNIK/REUTERS

Huku hayo yakiarifiwa rais Putin amekutana na maafisa wa juu wa Baraza lake la usalama, kujadili kuhusu usalama wa ndani wa taifa hilo, pamoja na kuchukua mikakati zaidi kujilinda na kile alichosema ni mashambulio ya makombora kutoka Ukraine.

Maafisa katika mji Kursk karibu na mpaka na Ukraine, walisema mashambulizi ya makom bora karibu na uwanja wa ndege yalisababisha moto mkubwa katika eneo la kuhifadhia mafuta.  Shamb ulizi hilo limekuja baada ya wizara ya ulinzi, kusema Ukraine inajaribu kushambulia uwanja mwengine wa ndege wa Ryazan na hata uwanja wa Engels katika mji wa Saratov.

soma zaidi: Urusi: Mafuta hayataathiri mashambulizi nchini Ukraine

Kwengineko Halmashauri ya Umoja wa Ulaya inafikiria kupiga marufuku uwekezaji katika sekta ya madini ya Urusi kama sehemu ya vikwazo vipya vinavyolenga kusitisha uwezo wa Urusi kufadhili vita vyake dhidi ya Ukraine.

Kulingana na gazeti la Financial Times marufuku hiyo itakuwa sehemu ya tisa ya vikwazo vya Umoja wa Ulaya ambako maafisa wa Halmashauri hiyo wanatarajia kuijadili na nchi wanachama katika siku kadhaa zijazo.

Vyanzo: reuters/afp/ap

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW