1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAJA CASABLANCA YA MOROCCO YATAWAZWA MABINGWA WA KOMBE LA CAF LA AFRIKA

24 Novemba 2003

- MKENYA PETER KORIR AWIKA KATIKA MBIO ZA MARATHON ZA SAN SEBASTIAN - AFRIKA KUSINI YAIPONGEZA UINGEREZA KWA KUTAWAZWA MABINGWA WA DUNI A KOMBE LA RUGBY

Kaiserslauten ilitia mabao 4 jana -3 kutoka mshambulizi wao Miroslav Klose na kufuta mabao 2 ya Hertha Berlin na mwishoe kutoroka na ushindi wa mabao 4-2. Jumamosi mabingwa bayern Munich walitokwa na jasho kabla ya kuondoka uwanjani na ushindi wa bao 1:0 dhidi ya mahasimu wao wa mtaani Munich 1860.Ushindi huo lazima uwatie shime Bayern munich kwa changamoto yao ya kesho ya champions League-Kombe la klabu bingwa barani ulaya kati yao na Celtic ya Scotland-ambayo imetia fora mwishoni mwa wiki kwa kuizaba Dundee mabao 5-1 katika Ligi ya Scotland.

Bayern munich iko nafasi ya 4 katika ngazi ya Bundesliga na hivyo pointi 6 nyuma ya viongozi wa Ligi Stuttgart. Munich inayocheza kesho na Celtic imo mashakani kuhusu stadi wao wa Brazil Ze Roberto.Riberto alirejea Munich kutoka Brazil ijumaa baada ya kuichezea Brazil katika changamoto za kuania tiketi ya kombe lijalo la dunia na akiwa na maumivu ya mgongo na kwahivyo kuna hofu ya kuweza kucheza kesho.

Stuttgart mwishoni mwa wiki hii iliizaba hannover mabao 3-1 na hivyo kurefusha rekodi yao ya kutoshindwa msimu huu hadi mechi 13.Huo ukawa ushindi wao wa 10 msimu huu. Werder Bremen imeangukia nafasi ya pili nyuma ya stuttgart huku bayer Leverkusen ikibidi kuridhika na nafasi ya 3.Bremen iliishindilia Bochum mabao 3-1.Leverkusen na Borussia Dortmund iliopo nafasi ya 5zilimudu suluhu mabao 2:2.

Mkiani mwa Ligi imesalia FC Cologne ambayo imeshindwa tena kuwika nyumbani na tangu kuanza msimu huu imejipatia ushindi 1 tu dhidi ya Borussia Dortmund. Orodha ya watiaji magoli inaongozwa na mbrazil Ailton-mshambulizi wa Werder Bremen aliekweishatikisa wavu mara 13 anafuatwa na Moroslav klose alietia jana pekee mabao 3 katika ushindi wa mabao 4-2 wa Bremen dhidi ya Berlin.

Katika changamoto za Kombe la shirikisho la dimba la Afrika-CAF: Raja Casablanca ya Morocco ilichachama jana na kumudu kutoka sare 0:0 na Contonsport Garoua ya Kamerun na hivyo imetwaa Kombe la CAF-la shirikisho la dimba la Afrika lililoaniwa kwa mara ya mwisho.Katika duru ya kwanza casablanca iliongoza kwa mabao 2:0 na jana ilitosha kwao kutoka suluhu huko Garoua,kamerun kutoroka na Kombe . Ushindi wa raja unatokana na juhudi kubwa aliofanya kipa wao Mustapha Chadli langoni.

LA RUGBY LIMEKWENDA UINGEREZA: Afrika kusini ambayo ilitolewa katika hatua ya robo-finali imeipongeza Uingereza kwa ushindi huo kabla mabingwa hao kuwasili kesho nyumbani Uingereza kwa mapokezi makubwa .Vyombo vya habari vya Afrika kusini vimehanikiza lakini kuikosoa Springboks-timu ya rugby ya nyumbani kwa jinsi ilivyocheza na uongozi mzima wa timu hiyo .

Patashika ilifikia kilele chake wiki iliopita baada ya kuibuka ripoti na picha za kambi ya mazowezi ambamo timu ya springboks ilikumbana na misukosuko mbali mbali wakati ikijiandaa kwa Kombe la dunia.gazeti la jana la Sunday Times limeitisha kuchukuliwa hatua haraka kupambana na hali mbaya iliozuka. Magazeti ya Afrika kusini alao yalitiwa moyo na jinsi Uingereza ilivyotamba na kutawazwa mabingwa wa dunia kwa ushindi dhidi ya Australia. Tumalizie RIADHA: Mkenya Peter Korir alishinda jana mbio za marathon za sab Sebastian nchini Spain akichukua muda wa masaa 2:10:46.Korir alimaliza kiasi cha dakika 5 kabla ya mshindi wapili,mkenya Paul Bor.Kenya kwakweli imezoa nafasi zote tatu baada ya David Maiyo kumaliza 3. Chama cha riadha ulimwenguni-IAAF kimethibitisha jana huko berlin kuwa,mji wa Fukuoka wa japan, ndio utakaoanda mashindano ya 34 ya ubingwa wa dunia wa mbio za nyika hapo april,2006. Moscow itaandaa mashindano ya ubingwa wa dunia wa ukumbini wa riadha 2006.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW